WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ametangaza rasmi kutokugombea tena (kustaafu) Ubunge wa Jimbo la Ruangwa, Lindi baada ya kulitumikia kwa muda wa miaka 15 mfululizo tangu mwaka 2010.
Hata hivyo, siku chache zilizopita akiwa Bungeni, mnamo Juni 26, 2025 Waziri Majaliwa alitangaza kuwa anapanga kugombea tena ubunge wa jimbo la Ruangwa akisisitiza kuwa anaendelea kuhitaji ridhaa ya wananchi wa Ruangwa.