WAKILI JUDITH KAPINGA AZIDI KUWA KIVUTIO KWA WANANCHI

Mgombea wa nafasi ya ubunge Jimbo la Mbinga vijijini Mkoani Ruvuma WAKILI JUDITH SALVIO KAPINGA (Kibonge mweusi) Leo oktoba 3-2025 ameendelea kufanya mikutano ya kampeni katika Kijiji Cha unango, Ngima na njombe vilivyopo Kata ya Ngima, Halmashauri ya wilaya ya Mbinga.

Ndugu JUDITH KAPINGA akiwahutubia wananchi wa vijiji Hivyo Maarufu Kwa kilimo Cha kahawa na ngano amewaomba ifikapo oktoba 29 wakichague chama Cha Mapinduzi na wagombea wake wa nafasi ya Urais Dokta SAMIA SULUHU HASSAN, ubunge Jimbo la Mbinga vijijini Ndugu JUDITH KAPINGA na udiwani Kata ya Ngima Ndugu Mwl. ADOLF KOMBA Ili waweze kutatua vyema kero za Maendeleo zinazowakabili ikiwemo Uboreshaji wa huduma ya Elimu, afya, umeme, Barabara, mawasiliano, kilimo, soko la kahawa n.k

Nae mgombea udiwani Kata ya Ngima Mwl. ADOLF KOMBA amewaomba wananchi wa Kata hiyo kukichagua  chama Cha Mapinduzi na wagombea wake wote wa Urais, ubunge na udiwani, kwani CCM  ndio chama pekee chenye uwezo wa kuwaletea Maendeleo wanangima na watanzania Kwa wote.

Upande wake Mwl. Prosper KAPINGA akizungumza Kwa niaba ya wananchi wote wa Kata hiyo amesema tayari CCM imeshashinda uchaguzi Mkuu kinachosubiliwa ni tarehe rasmi ya oktoba 29 kupiga kura ya ndio Kwa Rais, mbunge na diwani wote wa chama Cha Mapinduzi CCM.

Imetolewa na:
Cde. Angelo Joseph Madundo
Mratibu wa Kampeni za CCM uchaguzi Mkuu Jimbo la Mbinga vijijini 
      03/10/2025.





Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form