Ameandika Rais wa Heshima wa timu ya Simba Mo Dewji kupitia ukurasa wake wa #instagram 👇
"Wapenzi wa Simba,
Najua
mioyo yenu imebeba maswali mengi. Kama Rais wenu, msione nimekaa kimya
wakati tumepitia kipindi hiki kigumu. Kupambania Simba ni wajibu wangu.
Huu siyo wakati wa lawama - ni wakati wa kusimama imara, kuwa kitu kimoja, na kuchukua hatua sahihi za kuleta mabadiliko chanya.
Katika siku chache zijazo, nitazungumza na nyie moja kwa moja. Kuna kazi kubwa inaendelea, na kuna matumaini ya kweli.
Simba
haijapotea. Tumekuwa kwenye kipindi cha mpito tumejenga kikosi kipya,
tumeimarisha benchi la ufundi, na tumeweka msingi wa mwelekeo mpya.
Msimu huu tumefika mbali zaidi ya matarajio, na msimu ujao tunarudi kwa
nguvu mpya.
Naomba tuendelee kuwa wavumilivu. Tunahitaji kufanya marekebisho makubwa. Tuendelee kusimama pamoja kama familia moja.
Mbele yetu kuna mwanga. Na kwa pamoja, tutarudi tukiwa imara zaidi, wenye njaa zaidi, na wa kishujaa zaidi"
Tags
Michezo
