GAMONDI APEWA MASHARTI HAYA KUINOA SINGIDA BLACK STARS

Klabu ya Singida Black Stars imefikia makubaliano rasmi na kocha kutoka Argentina, Miguel Gamondi, ambaye sasa ndiye kocha mkuu mpya wa timu hiyo. 

Mkataba kati ya pande hizo mbili umesainiwa kwa njia ya kielektroniki na tayari umerejeshwa kwa uongozi wa klabu, ukithibitisha uamuzi huo mkubwa kuelekea msimu mpya wa mashindano.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani, Gamondi atawasili nchini Tanzania tarehe 22 Julai 2025, huku maandalizi ya msimu (pre-season) yakipangwa kuanza rasmi Julai 25. 

Gamondi anarudi tena katika ardhi ya Tanzania akiwa na dhamira ya kuiongoza Singida Black Stars katika kampeni za Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF Confederation Cup). Mashabiki wa timu hiyo wanatazamia mafanikio makubwa chini ya uongozi wake, hasa kutokana na uzoefu wake wa kimataifa na rekodi ya mafanikio katika vilabu mbalimbali barani Afrika ikiwemo klabu ya Young Africans FC.



Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form