YANGA YATANGAZA NEEMA KWA WANACHAMA WAO

 Uongozi wa Yanga SC umetangaza kuwa hii ni Wiki ya Mwisho kwa Mwaka wa Fedha ndani ya timu hiyo ya Mtaa wa Twiga na Jangwani, Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Masoko, Mashabiki na Wanachama wa timu hiyo Ibrahim Samuel amesema “ Hii ni Wiki ya Mwisho kwa Mwaka wa Fedha kwetu sote wana Yanga SC.

“June 30,2025 ndiyo itakuwa tamati ya makusanyo yote ya ADA kwa wanachama kabla ya kuukaribisha mwaka wetu wa Fedha ifikapo July 1,2025” alisema Ibrahim.

Ibrahim aliongeza kuwa “Kama mwanachama utakuwa bado haujalipa ADa yako mpaka June 30 basi utalazimika kulipa na msimu unaofuata ifikapo July 1,2025 kama Ibara ya 13:3 ya katiba ya klabu yetu inavyoelekeza.

Alifafanua kuwa “ Kama tawi lako litashindwa kufikisha wanachama НАI 100+ hadi June 30,2025, basi litakosa uwakilishi wa viongozi watano katika mkutano Mkuu wa msimu 2024 - 2025 kama Ibara ya 62 ya katiba yetu inavyoelekeza.

“ Na hii ndio tofauti ya Yanga SC na vilabu vingine vyote vya Afrika Mashariki, kati na Kusini” alisema Ibrahim.

Mkurugenzi huyo ametoa kauli Mbiu ya ulipaji Ada ya Mwanachama na kusema ADA ndio nguzo Mama ya Maendeleo kwa klabu yao.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form