Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na
Mwenza wake Mama Mbonimpaye Mpango wameungana na waumini mbalimbali wa
Kanisa Katoliki Duniani kushiriki Dominika ya Ekaristi Takatifu katika
Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohana wa Laterano lililopo Roma nchini Italia.
Misa hiyo imeongozwa na Baba Mtakatifu - Papa Leo XIV.