MKONGWE wa muziki wa R&B, Robert Kelly maarufu kama R.Kelly, amekataliwa ombi lake la kuachiwa kutoka gerezani siku chache baada ya mawakili wake kudai kuwa alizidishiwa dawa kutokana na njama ya kumuua iliyokwama.
Timu ya mawakili wa nyota huyo wa zamani wa R&B iliwasilisha ombi Juni 17, ikitaka apewe kifungo cha nyumbani badala ya kusalia gerezani kutokana na 'tishio la moja kwa moja la maisha yake.'
Hata hivyo,
Jaji Martha Pacold ameamua kuwa 'hakuna msingi wa kisheria kwa mahakama
kushughulikia ombi hilo' na kulitupilia mbali.
Mawakili wa Kelly
walidai wiki iliyopita kuwa msanii huyo alizidishwa dawa baada ya
walinzi wa gereza kumpa makusudi dozi kubwa ya dawa kupuga wasiwasi na
maumivu.
Pia walidai R. Kelly mwenye umri wa miaka 58, ambaye
jina lake halisi ni Robert Sylvester Kelly aliondolewa hospitali kwa
nguvu licha ya madaktari kugundua kuwa kulikuwa na tatizo kwenye damu
yake na miguuni ambako anatakiwa kufanyiwa upasuaji.
Waendesha
mashtaka wa serikali walikataa madai hayo wakati huo wakisema ni 'mambo
yasiyo na maana' na wakasema ombi la hivi karibuni linadhihaki mateso
waliyopitia waathirika matukio ya unyanyasaji wa ngono ambayo nyota huyo
aliyafanya enzi zake.
Hata hivyo, mawakili wake walidai, 'kila
muuaji, mbakaji na gaidi aliyepatikana na hatia atakuwa na nafasi mpya
ya kupata uhuru' kama Kelly angeachiwa. Pamoja na hilo na kukataliwa kwa
ombi la kifungo cha nyumbani, wakili wake Beau Brindley alisisitiza
kwamba yeye na timu yake ya sheria wangewasilisha ombi jipya wakidai
kuwa kuna 'ushahidi mpya uliogunduliwa.'
Brindley alisema ombi
hilo pia litaomba dhamana ya haraka wakati shauri hilo likiendelea na
kwamba, " Hatukushangazwa na uamuzi huu kwa kuwa tulijua kuwa suala la
mamlaka ya kiufundi lingekuwa changamoto katika mazingira haya."
Brindley
akizungumza na USA TODAY, alisema: "Awali, hata hivyo, hatukuwa na
chaguo bali kuchukua hatua mara moja kutokana na ushahidi wa wazi wa
tishio kwa maisha ya Robert Kelly."
Tags
Burudani