Wakati
mapigano kati ya Israel na Iran yakiingia siku ya kumi na moja, Mahakama
ya Nchini humo imemhukumu kunyongwa mtu mmoja aliyepatikana na hatia ya
kufanya ujasusi wa Israel.
Kwa mujibu wa Taarifa ya Idara ya
Mahakama ya Iran imeleza kuwa mtu huyo aliyefahamika kwa jina la
Mohammad- Amin amenyongwa siku ya leo Jumatatu. "Mohammad-Amin
Mahdavi Shayesteh alinyongwa asubuhi ya leo kwa ushirikiano wa kijasusi
na utawala wa Kizayuni," ilisema Idara ya Mahakama.
Shayesteh alidaiwa kuwa na uhusiano na Mossad, shirika la kijasusi la kigeni la Israel.
Pia
alikutwa na hatia ya kushirikiana na Iran International, kituo cha
televisheni cha lugha ya Kiajemi kilichoko London ambacho kinaikosoa
serikali ya Iran.