Katibu Mkuu
wa Umoja wa Vijana wa CCM, Ndugu Jokate Urban Mwegelo (MNEC) amesema
Amesema, Daraja hili halihusiani tu na usafiri au Usafirishaji, bali
daraja hili ni Fursa. Kwetu sisi Vijana tunaiona miradi hii kama fursa
ya Ajira za muda mfupi na muda mrefu, kuongeza masoko ya kibiashara,
fursa za kidigitali na Ubunifu.
Ndugu Jokate ameyasema hayo jana
juni 22, 2025 katika Kongamano la Jukwaa la Fikra lililoandaliwa na
Mwananchi Communications Limited (MCL) kwa kushirikiana na Wizara ya
Ujenzi, lililojadili mada isemayo, 'Kujenga Madaraja, Kujenga Taifa,
Miundombinu kama Kichocheo cha Ukuaji JumuishiNdugu Jokate
agusia namna Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025/30 ilivyojielekeza
kugusuia mambo ya Kimkakati na kuigusa jamii katika ngazi ya msingi.
“Mimi nadhani ni wakati sasa wa kuwa na mpango wa Taifa wa kuwezesha
Vijana kushiriki katika miradi ya ujenzi wa miundombinu ya Tanzania”.
Pamoja
na hayo, Ndugu Jokate ampongeza Rais Samia kuwa; “Rais Samia ni
kielelezo na tafsiri halisi ya neno Kiongozi kwa sababu hakua mbinafsi
ameweka maslahi ya Taifa mbele, na hili kwetu sisi Vijana lazima
tujifunze; ametufundisha kwamba unaweza kuwa Kiongozi Mwanamke, Msikivu,
Madhubuti lakini pia mwenye uthubutu wa kufanya maamuzi magumu.”
0 Comments