MAPOROMOKO YA ARDHI YAUA MAELFU SUDAN

 Takriban watu 1,000 wamepoteza maisha kutokana na maporomoko ya ardhi katika milima ya Marra, magharibi mwa Sudan, kufuatia mvua kubwa zilizonyesha katika mkoa wa Darfur. Mtu mmoja pekee ameripotiwa kunusurika.

Kwa mujibu wa Vikosi vya Ukombozi wa Sudan (SLM/A), kijiji kilichoathirika ambacho kilikuwa makazi ya wakimbizi wa ndani waliokimbia mapigano ya Darfur Kaskazini kimezama kabisa ardhini. Juhudi za uokoaji zinatatizwa na hali ngumu ya kijiografia na ukosefu wa vifaa.

SLM/A imetoa wito kwa Umoja wa Mataifa na mashirika ya kimataifa kutoa msaada wa haraka kwa manusura na kusaidia kutafuta miili ya waathirika.

akriban watu 1,000 wamepoteza maisha kutokana na maporomoko ya ardhi katika milima ya Marra, magharibi mwa Sudan, kufuatia mvua kubwa zilizonyesha katika mkoa wa Darfur. Mtu mmoja pekee ameripotiwa kunusurika.

Kwa mujibu wa Vikosi vya Ukombozi wa Sudan (SLM/A), kijiji kilichoathirika ambacho kilikuwa makazi ya wakimbizi wa ndani waliokimbia mapigano ya Darfur Kaskazini kimezama kabisa ardhini. Juhudi za uokoaji zinatatizwa na hali ngumu ya kijiografia na ukosefu wa vifaa.

SLM/A imetoa wito kwa Umoja wa Mataifa na mashirika ya kimataifa kutoa msaada wa haraka kwa manusura na kusaidia kutafuta miili ya waathirika.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form