Kwa sasa Yanga tuna ajenda moja tu, ambalo ni Tamasha bora na kubwa AFRIKA la 𝐖𝐢𝐤𝐢 𝐲𝐚 𝐌𝐰𝐚𝐧𝐚𝐧𝐜𝐡𝐢 na kila mwananchi atafurahi, tukio la msimu huu lazima liwe na huduma rafiki kwa familia na kila mtu. Tunahakikisha tunatoa huduma bora kuwahi kutokea katika historia ya matamasha ya michezo Tanzania”
“Tunatarajia kuwa na burudani kubwa na ya kipekee kutoka kwa wasanii wakubwa sana, tumeshaongea na wasanii husika tumewaeleza kuwa wanapaswa kupandisha daraja lao la burudani. Kila mwanayanga atakayefika uwanjani atakutana na burudani ambayo hajawahi kuipata popote”
“Tutakuwa
na mchezo wa timu ya Yanga Princess siku ya Kilele cha 𝐖𝐢𝐤𝐢 𝐲𝐚
𝐌𝐰𝐚𝐧𝐚𝐧𝐜𝐡𝐢, Yanga Princess msimu huu ni moja kati ya timu ambayo
tumefanya usajili bora sana. Tumeonesha jeuri ya fedha. Tumemrejesha
Precious, Wincate na Mynaco. Tumehakikisha wachezaji wetu bora kama
akina Aregash wamesalia. Mratibu wa Yanga Princess amesema hakuna tena
kisingizio”
“Tutakuwa na mchezo mwingine muhimu sana wa timu ya
viongozi wa Yanga na wasanii, huu utakuwa mchezo wa kukata na shoka.
Mechi ya mwisho nilitokea benchi ila mchezo huu nitakwenda kuanza na
wasipokuwa makini nitachukua na kitambaa kabisa. Kocha wetu Romain Folz
na msaidizi wake Rodriguez nao watakuwepo”
“Uzinduzi wa kuelekea 𝐖𝐢𝐤𝐢 𝐲𝐚 𝐌𝐰𝐚𝐧𝐚𝐧𝐜𝐡𝐢 utafanyika kesho katika viwanja vya Zakhiem, tunataka kufanya maandamano makubwa na ya kihistoria, tunataka DSM nzima iwe kijani na njano, kuanzia majira ya saa tano kila mtu afike Zakhiem Mbagala. Mwenye baiskel, mwenye daladala, mwenye pikipiki kesho ni historia ya mpira inaenda kuzinduliwa, tutatambulisha baadhi ya wasanii watakaokuwepo 𝐒𝐢𝐤𝐮 𝐲𝐚 𝐌𝐰𝐚𝐧𝐚𝐧𝐜𝐡𝐢”
“Leo tumefanya mkutano wa kwanza kuelekea siku ya Mwananchi, lakini tayari tumeshauza tiketi zote za VIP A. Kimsingi tamasha hili limeshavuka kuwa tamasha la michezo ni Tamasha la kihistoria, kama hujanunua tiketi mpaka sasa una dalili za kupoteza fursa adhimu ya kushuhudia kilele cha wiki ya Mwananchi”
“Wanayanga sasa wamevuka level ya kuwa na Slogan za kupeana matumaini, tumekubaliana huu ni msimu wa vitendo na tumegundua watu bado wanataka dozi, kuanzia sasa tunaenda kupiga kichwani tu. Hiyo ndio slogan yetu, Tukipiga kichwani tunacheza na ufahamu. Mwaka huu ni kichwa tu, tumeweka kabisa nyundo kwa ajili ya wale wanaokaza fuvu”
Tags
Michezo
