WANANCHI RONDO-LINDI WAMSHUKURU RAIS SAMIA KWA MRADI WA MAJI SAFI

 Wananchi wa Rondo Jimbo la Mtama wilayani Lindi wamemshukuru Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia Mkuu wa Wilaya ya Lindi Victoria Mwanziva alipofika na kufanya ziara ya Ukaguzi wa mradi wa mkombozi wa maji Chikombe- Mkanga 2, Tarafa ya Rondo, Jimbo la Mtama- Halmashauri ya Mtama.

Jumla ya wakazi 2823 kutoka katika vijiji vya Chikombe na Mkanga Il vilivyopo Tarafa ta Rondo, Kata ya Mnara- Halmashauri ya Mtama, wanatarajia kupata neema kubwa ya upatikanaji wa maji safi, salama na yenye kutosheleza muda wote. 

Wizara ya Maji kupitia Wakala wake wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Lindi kwa kushirikiana na Kanisa Anglikana Tanzania Dayosisi ya Masasi chini ya ufadhili wa shirika la Grille Foundation wanatekeleza mradi wa maji wa Chikombe-Mkanga Il ambao ni wa upanuzi wa miundombinu kutoka mradi mkubwa wa Rondo kwaajili ya kuwahudumia wananchi wote. 

Wananchi wa Rondo- wameshiriki katika hatua zote za utekelezaji wa mradi huu haswa kwenye mazoezi ya ufukiaji wa mabomba, na wameahidi utunzaji wa miundombinu ya maji ya mradi huu ambao unatazamiwa kukamilika hivi karibuni. 
Wana-Mtama wanazidi kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa za kuchagiza maendeleo katika Sekta zote za Afya, Elimu, Maji, Miundombinu.







Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form