RAIS SAMIA ASEMA DENI LA TANZANIA NDIO DOGO AFRIKA MASHARIKI

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Taifa la Tanzania mpaka kufikia 2024 ndilo deni dogo la taifa dogo kwa ukanda wa Afrika Mashariki ukilinganisha na wastani wa deni hilo kwa nchi zote za Afrika Mashariki.

 Dkt. Samia Ameyasema hayo hii leo Agost 28, wakati akizungumza katika ufunguzi wa kampeni za Chama cha Mapinduzi (CCM) kitaifa zilizozinduliwa katika viwanja vya Tanganyika Pakers, Jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa deni zima la mataifa yote duniani limefika asilimia 93.

“Ndugu wananchi deni la taifa hadi kufikia mwaka 2024, Deni la serikali zote duniani lilikuwa asilimia 93 ya pato lote la dunia ukichukua serikali zote za dunia, wakati pato la serikali zote za Afrika lilikuwa silimia 67 ya pato lote ndani ya bara la Afrika, kwa ukanda wa Afrika Mashariki deni hili lilifika asilimia 67 kwa wastani wa pato la taifa kwa nchi zote za Afrika Mashariki”

“Wakati tukienda kwa nchi Moja moja hapa kwetu nchini Tanzania lilisalia kuwa asilimia 46 ya pato letu la taifa na hili ndio deni dogo kuliko yote kwa nchi za Afrika Mashariki, Asilimia 46 ukilinganisha na washtani wa asilimia 67” Amesema Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form