Wakala wa
Nishati Vijijini (REA) umepongezwa kwa utekelezaji wa Mradi wa Mkopo
Nafuu wa Ujenzi wa Vituo Vidogo vya Bidhaa za Mafuta (Petroli na Dizeli)
Vijijini ambapo utekelezaji wake umetajwa kuwa kichocheo cha maendeleo
ya Watu wa vijijini.
Akitoa pongezi hizo; Katibu Tawala wa wilaya
ya Ikungi, Bwana Rashid Rashid ambaye ametembelea banda wa REA leo,
Agosti 4, 2025 katika viwanja vya Nane Nane, Nzuguni, Jijini Dodoma. Bwana
Rashid amesema huduma ya usafiri wa Watu wa vijijini inategemea nishati
ya mafuta ya dizeli na petroli na kwamba kusogeza karibu na Wananchi
huduma ya nishati ya mafuta; kutarahisisha usafiri kwa Watu na mazao ya
kilimo ambapo bado maeneo mengi Wananchi wanalazima kusafiri umbali
mrefu kufuata huduma mbalimbali za kijamii.
Wakati huo huo; wito
umetolewa kwa Wananchi wanaotembelea Maonesho ya Kimataifa ya Nane Nane
2025 kufika banda la Wakala (REA) ili kujifunza kuhusu upatikanaji wa
teknolojia za nishati safi ya kupikia; fursa ya utoaji wa mikopo nafuu
ya ujenzi wa vituo vidogo vya bidhaa za mafuta (Petroli & Dizeli)
vijijini; usambazaji wa umeme kwenye vijiji na vitongoji.
Ambapo
imeelezwa kuwa watapata elimu kuhusu vigezo vya namna ya kupata mkopo
huo nafuu na wenye sifa watapata fursa ya kujaza fomu za maombi ambazo,
zinapatikana katika Banda la REA bila gharama yoyote.
Banda la
REA lipo kwenye eneo la Wizara ya Nishati katika hema namba (2) la
Serikali yaani (Government Pavilion; No. 2); upande wa Kusini Mashariki
wa viwanja vya Nzuguni, Jijini Dodoma.