Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Salim Abri Asas, ameshiriki zoezi la kura za maoni katika kata yake ya Gangilonga, ikiwa ni sehemu ya mchakato wa ndani wa chama hicho unaofanyika nchi nzima kwa ajili ya kuwapata wagombea wa nafasi za udiwani, ubunge na uwakilishi kwa Zanzibar, kufuatia marekebisho ya Katiba ya CCM ya mwaka 1977.
MCC
Asas amelitumia zoezi hilo kuwataka wanachama wa CCM kote nchini
kutekeleza haki yao ya kidemokrasia kwa kushiriki kikamilifu ili
kuwachagua viongozi bora watakaoisimamia ilani ya chama kwa ufanisi.
Amesisitiza kuwa ilani hiyo imejikita katika kutatua changamoto
mbalimbali za wananchi, na hivyo uchaguzi wa viongozi sahihi ni hatua
muhimu kuelekea maendeleo ya kweli.