RAIS SAMIA ATOA BILIONI 221 UJENZI WA BARABARA SHINYANGA

 Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt @samia_suluhu_hassan ametoa zaidi ya Bilioni 221 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya barabara za Shinyanga ikiwemo,madaraja na makalvati ili kuwezesha shughuli za kiuchumi na kijamii.

Kupitia fedha hizo, mtandao wa barabara za lami umeongezeka kutoka kilomita 224 mwaka 2020 hadi kilomita 281 mwaka 2025, barabara za changarawe kutoka kilomita 957.11 hadi 1,411.50, madaraja kutoka 45 hadi 57, na makalvati kutoka 2,356 hadi 4,469. Aidha, taa za barabarani 611 zimesimikwa ili kuboresha usalama wa watumiaji wa barabara hasa nyakati za usiku.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form