Mwanasiasa mkongwe na aliyewahi kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina, amejiunga rasmi na chama cha upinzani cha ACT Wazalendo, hatua inayotajwa kuibua mvutano wa kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Mpina,
ambaye alihudumu kama Mbunge wa Jimbo la Kisesa kwa tiketi ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM) kwa miaka kadhaa, ameonekana katika picha na video
zilizosambaa mitandaoni, akijiandikisha kupitia mfumo rasmi wa chama
hicho uitwao Kiganjani, mbele ya Naibu Kiongozi wa ACT Wazalendo –
Taifa, Dorothy Semu. Taarifa hizo sasa zimethibitishwa na uongozi wa
chama hicho.