Askofu wa Makanisa ya Ufufuo na Uzima nchini Tanzania Josephat Gwajima ametoa siku 10 kwa mamlaka nchini kuondoa zuio la makanisa hayo kuendesha shughuli zake.
Akizungumza kupitia televisheni ya mtandaoni usiku wa siku ya Ijumaa , Gwajima ameeleza kuwa makanisa hayo yalifungwa pasina kufuata misingi ya haki hivyo kuwasababishia adha waumini wa makanisa hayo.
“Leo ni tarehe 15 Agosti, tarehe 24 hivi au 25 Septemba nitarudi tena na nitazungumza jambo ambalo kila atakayesikia atastaajabu”, ameeleza Gwajima