Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele, leo tarehe 15 Agosti 2025 amekabidhi fomu za uteuzi kwa mgombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Luhaga Joelson Mpina, na mgombea wa kiti cha Makamu wa Rais, Fatma Abdulhabib Ferej, kupitia Chama cha ACT Wazalendo.