WANANCHI HAI WANUFAIKA NA MRADI WA AFYA WA 209.6

Wananchi wa Kijiji cha Mtakuja, Kata ya Kia, Wilaya ya Hai – Kilimanjaro sasa wanapumua kwa matumaini baada ya Serikali kujenga jengo la OPD katika Kituo cha Afya Kia kwa gharama ya Shilingi Milioni 209.6.

Mwenge wa Uhuru umeweka jiwe la msingi kuashiria uzinduzi wa huduma hiyo muhimu.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Hai, Dkt. Itikija Msuya amesema fedha hizo zilitolewa na Halmashauri kupitia mapato ya ndani, huku wananchi wakichangia Milioni 6.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025, Ndg. Ismail Ali Ussi amesema mradi unaendana na thamani ya fedha iliyotumika, na kuutaka umma kuulinda kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.

Mwenge wa Uhuru ukiwa Hai umefungua na kuzindua miradi 7 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 3.63.








Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form