Sakata la mchezaji Stephanie Aziz Ki limechukua sura mpya huko Wydad Casablanca baada ya sintofahamu kuibuka juu ya yeye kuendelea kuchezea timu hiyo au kuna jambo lingine litaendelea.
Meneja habari na mawasiliano wa
klabu ya Yanga SC, Ali Kamwe ametoa ufafanuzi juu ya mkataba wa kiungo
huyo Aziz Ki na klabu ya Wydad Casablanca na kueleza kuwa makubaliano
yao ilikuwa ni kuwatumikia Wydad kwa mkataba wa miezi mitatu.
Ali
Kamwe ameweka wazi kwamba, mkataba huo una vipengele viwili ambapo
ikiwa Wydad Casablanca itaridhishwa na kiwango chake basi watamuongezea
mkataba wa miaka miwili na ikiwa tofauti na hapo atarejea ndani ya Yanga
SC na kuendelea na mashindano mwingine.
Yanga SC na Wydad
walikubaliana hadi kufikia Julai 10, wawe wameshawasiliana ili kuona
kama kuna kuongeza mkataba au kuishia hapo.
Tags
Michezo
