Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.
Ridhiwani Kikwete ametembeela banda la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa
Watumishi wa Umma PSSSF kwenye Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa
ya Dar es Salaam na kujionea jinsi wanachama na wananchi
wanavyohudumiwa.
Mhe. Kikwete ambaye aliambatana na Naibu Waziri
Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.
Patrobas Katambi, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana,
Ajira na Wenye Ulemavu, Bi. Zuhra Yunus, alielezwa jinsi wanachama na
wananchi wanavyohudumiwa katika banda hilo.
Alifurahishwa na
taarifa ya namna wanachama wanavyofurahia huduma za PSSSF Kidijitali
ambazo zimepelekea mapinduzi makubwa katika utoaji wa huduma.
Pia
Mhe. Kikwete alijionea bidhaa bora za viatu, mikoba na mikanda
vinavyozalishwa kwenye kiwanda cha KLICL ambacho PSSSF imewekaza.