SEKTA YA AFYA.
Kipindi cha awamu ya sita ndani ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025 Jimbo la Morogoro Mjini limepata neema ya kutekelezewa miradi mbalimbali ya Sekta Afya kwa ajili ya Wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro na kutumia kiasi cha Tsh Bil. 9,094,891,580.23 kwa ajili ya ujenzi wa miradi mipya na uboreshaji wa huduma za afya kama ifuatavyo:-
Ujenzi wa Hospitali mpya ya Wilaya yenye thamani ya Tsh Bil. 2,890,000,000.00 ambapo jengo la wagonjwa wa nje (OPD),Maabara, jengo la Wazazi na upasuaji, jengo la mionzi, jengo la kufulia, jengo la kuhifadhia maiti, jengo la kuhifadhia dawa, wodi ya wanaume, wanawake na watoto vyote vimekamilika, vya kisasa na huduma inaendelea kutolewa katika hospitali hii.
Ujenzi wa Vituo viwili vikubwa vya Afya(Lukobe na Tungi) uliogharimu kiasi cha Tsh bil. 1,269,470,700.00 umekamilika na wananchi wanapata huduma, vituo hivi vimejitoshereza katika kila idara ya kimatibabu
Ujenzi wa Zahanati 16 zenye thamani ya Tsh bil 1,019,628,990.00 zimekamilika na zinatoa huduma mfano wake, ni zahanati ya kauzeni, u/taifa, mazimbu, sultan area, Tungi, Mbuyuni, kiwanja cha ndege, mji mkuu, lukobe n. k.
Uboreshaji wa Zahanati katika Halmashauri ya manispaa ya morogoro ambao umetumia kiasi cha tsh mil. 232 ili kusaidia kuweka miundombinu faafu ya zahanati itakayowezesha wananchi kupata huduma stahiki (kazi hii imefanyika kwa vitendo) mfano wake ni Zahanati ya mji mpya, mwembesongo, mafiga n.k
Uboreshaji wa Huduma ya mama na mtoto umefanyika katika zahanati (3) za Mwembesongo, Mji mpya, na Kihonda na aidha ujenzi wa ukuta zahanati ya mwembesongo na mji mpya umefanyika.
Ununuzi wa vifaa tiba na madawa katika hospitali ya wilaya, vituo vya afya na zahanati vyenye thamani ya tsh bil 4,207,242,923.4 umefanyika.
Katika kuboresha Miundombinu ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro vifaa ghari na muhimu vimenunuliwa na vinatumika vikiwemo city scan,mashine ya kusafisha figo, chumba wa wagonjwa mahututi (watu wazima na wodi ya watoto wanaozaliwa njiti na kuhitaji uangalizi maalum n.k, ununuzi wa ambulance 1 na magari 2 ya utawala ili kurahis huduma.
Aidha kwenye sekta hii ya Afya Mhe Abood amefanya mambo mengi kwa kutoa pesa zake binafsi kwa kuchangia michango mbalimbali kama vile ununuzi wa Ambulance 🚑 nne 4 kutoka kwenye pesa yake binafsi
Ndani ya kipindi cha awamu ya sita cha Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Huduma za Afya zimesogozwa karibu zaidi na wananchi kwa zaidi ya asilimia 97.
Asante sana Mhe Rais Samia Suluhu Hassani.
