Mkoa wa Dar
es salaam umedhamiria kuendelea kuimarisha miundombinu ya usafirishaji
wa mizigo na watu kwa kujenga barabara bora ili kuufanya Mkoa huo
uendelee kuwa kitovu cha uwekezaji na biashara na uendelee kuchangia
kwenye pato la nchi kwa asilimia kubwa.

Akizungumza leo Julai 10,
2025 Jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya Mkoa wa Dar es
salaam yaani "Dar es salaam Day" kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es
salaam Mkuu wa wilaya ya Temeke Mhe Sixtus Mapunda amesema Mkoa wa Dar
es Salaam ni kitovu cha biashara na unachangia kwenye mapato ya nchi kwa
asilimia 17 hivyo Mkoa unaendelea kuimarisha miundombinu ya barabara na
madaraja kwa ajili ya usafirishaji, ambapo amesema Mkoa huo unafursa na
maeneo mengi kwa ajili ya uwekezaji na biashara kwenye kila wilaya na
kwamba ubora wa Mkoa huo unachagizwa na kazi nzuri iliyofanywa na Rais
Dkt Samia Suluhu Hassan kuimarisha Bandari,Usafiri wa reli ya
kisasa,uwanja wa ndege pamoja uwepo wa huduma bora za umeme na maji.
Aidha
Mhe Mapunda ametoa mchanganuo wa maeneo ya uwekezaji kwa kila wilaya
ambapo Wilaya ya Temeke ni maeneo 17,kinondoni maeneo 29 Jiji la Dar es
Salaam maeneo 9, kigamboni maeneo 27 na ubungo maeneo maeneo 6 kwa ajili
ya uwekezaji.
Kwa upande waKatibu Tawala wa Mkoa wa Dar es
salaam Bwana Abdul Mhite amesema katika kuimarisha shughuli za biashara
na uwekezaji Mkoa huo umekuwa na mikakati mbalimbali ikiwemo kuanzisha
mfumo wa biashara saa 24 pamoja na kutoa mikopo ya asilimia 10 kwa
wafanyabiashara ambapo zaidi ya vikundi 2000 tayari vimepatiwa mikopo
Maadhimisho
ya siku ya Mkoa wa Dar es salaam yamefanyika kwenye viwanja vya
SABASABA huku yakijielekeza kwenye mkakati wa kutangaza fursa mbalimbali
za uwekezaji zilizopo katika Mkoa wa Dar es Salaam.