Rais
wa Mpito wa Mali, Assimi Goita, ametia saini sheria mpya inayompa
mamlaka ya kubaki madarakani kwa muda usio na kikomo. Sheria hiyo
imeondoa ukomo wa mihula ya urais na kuchelewesha uchaguzi mkuu, hatua
ambayo imeibua hofu kubwa miongoni mwa wakosoaji kuhusu mustakabali wa
demokrasia nchini humo.
Wapinzani na wanaharakati wa haki za
kiraia wanasema hatua hiyo ni kurudi nyuma kwa maendeleo ya
kidemokrasia, huku wakihofu kuwa Mali inaweza kutumbukia katika utawala
wa kiimla. Hadi sasa, haijabainika lini uchaguzi mpya utafanyika.
Goita,
alichukua madaraka kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka 2021, sasa
anashikilia mamlaka makubwa zaidi, huku jumuiya ya kimataifa ikitoa wito
wa kurudishwa kwa utawala wa kiraia.