Mahakama Kuu
ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali maombi ya
Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, aliyekuwa akitaka uamuzi wa Mahakama
ya Kisutu wa kuahirisha usikilizwaji wa kesi yake ya kuchapisha taarifa
za uongo mtandaoni upitiwe upya.
Katika uamuzi wake, Mahakama
Kuu imesema kuwa maombi hayo hayakuwa sahihi kufikishwa kabla ya kesi ya
msingi kukamilika, hivyo yamekataliwa kwa msingi wa kisheria.
Tundu
Lissu alikuwa anapinga uamuzi uliotolewa Juni 2, 2025, na Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu, lakini sasa atalazimika kusubiri hadi kesi ya
msingi itakapokamilika ndipo hatua zaidi ziweze kuchukuliwa.