MAKALLA ASEMA WATIA NIA WALIOCHANGISHWA FEDHA WARUDISHIWE

 Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla ameelekeza watia nia wa ubunge na udiwani waliolipishwa fedha za ziada wakati wa kuchukua fomu wilayani Meatu mkoani Simiyu kurudishiwa fedha zao.

Hatua hiyo imetokana na malalamiko yaliyotolewa na mtia nia ya ubunge Jimbo la Meatu kupitia CCM, John G’wanambuke kueleza kutakiwa kulipa TZS 500,000 ya ziada kwa ajili ya kugharamia kampeni za uchaguzi.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form