Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Kamati ya Halmashauri Kuu ya Chama hicho, imemteua Mkurugenzi Mtendaji wa Manara TV, @hajismanara , kuwa miongoni mwa wagombea watakao wania nafasi ya Udiwani katika Kata ya Kariakoo,Wilaya ya Ilala, Jijini Dar es Salaam.
Uteuzi
wa Manara umetokana na mchakato wa kina wa ndani wa chama ambapo
wagombea kadhaa walichujwa kwa mujibu wa taratibu na vigezo vilivyowekwa
na CCM.
Manara ameibuka miongoni mwa waliokidhi vigezo na
kuaminiwa na chama hicho ambapo wengine wagombea walioteuliwa kuwania
nafasi hiyo ni pamoja na Daudi Abdallah Simba,Abdulkarimu Massamaki.
Uamuzi
huu wa CCM pia unaonekana kuwa majibu kwa tetesi na mijadala iliyokuwa
imeenea mitandaoni na kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuhusu jina la
Manara kutokupitishwa na Kamati Kuu ya chama.
Uteuzi huu sasa unaweka wazi msimamo wa chama na kuondoa sintofahamu kwa wanachama na wafuasi wa CCM.
Haji
Manara si jina geni ndani ya chama hicho, akiwa amewahi kushika nafasi
mbalimbali za uongozi, ikiwemo kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM
Mkoa wa Dar es Salaam, nafasi iliyompatia umaarufu mkubwa kutokana na
ustadi wake wa kuwasiliana na wanachama pamoja na wananchi.
Mbali
na siasa, Manara anafahamika pia kwa mchango wake mkubwa katika tasnia
ya michezo nchini, hususan alipokua Msemaji mahiri wa vilabu Vikubwa
nchini Simba SC na Yanga SC.