Timu ya Fountain Gate FC imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji Stand United FC ‘Chama la wana’ katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa mtoano kati ya timu ya ligi kuu na ligi ya Championship, uliopigwa uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.
Mabao ya Fountain Gate FC katika
mchezo wa leo yamefungwa na Kassim Haruna (Kipindi cha kwanza), Sadick
Ramadhani na Mudrick Shehe (Kipindi cha pili) huku bao pekee la Stand
United FC likiwa ni la kujifunga kupitia kwa Jarom Mgeveke (Kipindi cha
kwanza).
Mchezo wa mkondo wa pili utapigwa Jumanne ya Julai 8
kwenye uwanja wa Tanzanite Kwaraa mjini Babati Mkoani Manyara, ambapo
mshindi wa jumla atacheza ligi kuu ya NBC Tanzania bara msimu ujao.
Tags
Michezo



