CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA JIJINI DAR ES SALAAM
byDarasa Huru-
Mkuu wa Mkoa
wa Dar es alaam Mhe Albert Chalamila amewataka wenyeviti wa Serikali za
mitaa pamoja na watendaji wa Kata Mitaa Mkoani humo kusimamia ulinzi na
usalama kwenye ngazi ya mitaa na kata ili kuhakikisha Mkoa huo unakua
Salama bila uwepo wa matukio ya uvunjifu wa amani wakati wote.
Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam katika kikao kazi na Wenyeviti, Watendaji wa
Kata na mitaa kilichofanyika kwenye ukumbi wa Diamomd Jubilee RC
Chalamila amesema suala la ulinzi na usalama linapaswa kuanzia kwenye
ngazi ya mitaa na kata hivyo amewataka viongozi hao wa mitaa kusimamia
suala hilo kwani katika baadhi ya mitaa kumekua na matukio ya uvunjifu
wa amani.
RC Chalamila amewataka viongozi hao ngazi ya Mitaa na
Kata kusaidia kutatua changamoto za wananchi na sio wao kuwa ni chanzo
cha kuongeza changamoto kwa wananchi ambapo pia ametumia nafasi hiyo
kuwataka wenyeviti na watendaji kutambua kuwa mwaka huu ni mwaka wa
uchaguzi hivyo waendelee kuhimiza wananchi kuanzia ngazi ya mtaa
kushiriki uchaguzi
Aidha RC Chalamila kupitia Kikao kazi hicho
amewataka wenyeviti wa mitaa pamoja na watendaji wa mitaa na Kata
kuhamasisha wananchi na wafanyabiashara kulipa kodi ili kuwezesha
Serikali kuwa na fedha za kutosha ili kuweza kutekeleza miradi
mbalimbali ya maendeleo, kwani Rais Dkt Samia anahitaji fedha ili
kuendelea kuleta maendeleo kwa masilahi mapana ya umma.
Aidha
ameongeza kuwa katika hotuba ya Rais wakati akiapisha viongozi hivi
karibuni Mkoani Dodoma aliwasisitiza wakuu wa mikoa mambo manne ikiwemo
umuhimu wa kulinda amani, kukusanya mapato kusimamia miradi ya maendeleo
pamoja na kushuka kwa wananchi kusikiliza kero zao hivyo ili kutimiza
hayo viongazi ngazi ya mitaa na kata wana nafasi kubwa.
kwenye ngazi ya mitaa na kata ili kuhakikisha Mkoa huo unakua