KIONGOZI WA MAPINDUZI MALI APEWA MUHULA WA MIAKA 5 MADARAKANI

 Kiongozi wa Kijeshi wa Mali, Jenerali Assimi Goïta amepewa muhula wa Urais wa miaka mitano na Bunge la mpito.Kiongozi huyo wa Kijeshi ambaye amenyakua Mamlaka mara mbili, aliahidi kurejea kwa demokrasia mwaka jana, lakini haikufanyika.

Kiongozi huyo wa Kijeshi mwenye umri wa miaka 41 aliteuliwa kuwa Rais wa mpito baada ya Mapinduzi yake ya mwisho mwaka 2021.

Wakati huo aliahidi kufanya uchaguzi mwaka unaofuata lakini tangu wakati huo alikataa,ikiwa ni pigo katika juhudi za kurejesha utawala wa vyama vingi.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form