BABA MZAZI WA SAMATTA AFARIKI DUNIA

NI huzuni kubwa katika familia ya mshambuliaji wa timu ya taifa 'Taifa Stars', Mbwana Samatta kufuatia taarifa za kifo cha baba mzazi, Ally Samatta.

Mzee Samatta amefariki dunia leo hii nyumbani kwake Mbagala Dar es Salaam na taarifa za kifo chake zimethibitishwa na mwanae, Mohamed Samatta.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa ndugu wa familia, Mzee Ally Samatta alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya kiafya.



Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form