Mageuzi
makubwa yaliyofanyika katika sekta ya elimu nchini, hususan mafunzo ya
Amali yameanza kuvutia mataifa mengine barani Afrika kuja kujifunza
namna yalivyofanyika na utekelezaji wake.

Hayo yamebainishwa
Julai 05, 2025 jijini Dodoma kufuatia ziara ya Waziri wa Elimu ya Juu,
Utafiti, Sayansi na Teknolojia kutoka Jamhuri ya Gambia Prof. Pierre
Gomez ambaye amesema lengo la kufika Tanzania ni kujifunza mbinu
zilizotumika katika kufanya maboresho na maugezi makubwa katika sekta
ya elimu.
Waziri huyo amesema kuwa Benki ya Dunia iliishauri nchi
hiyo kuja Tanzania ili kujionea namna utekelezaji wa Sera, mikakati na
miradi mbalimbali katika sekta ya elimu ili kuwawezesha kutekeleza
miradi yao kwa ufanisi na tija.
“Tumeshuhudia ujenzi wa
miundombinu na mifumo ya mafunzo ya vitendo yenye tija katika vyuo
mbalimbali ikiwemo DIT, VETA na Taasisi, tunaamini kunufaika zaidi
kupitia ushikiano katika nyanja mbalimbali za mafunzo" Alisema Prof.
Gomez.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Tanzania Prof.
Adolf Mkenda amesema Tanzania iko tayari kushirikiana na Gambia katika
kubadilishana wakufunzi na wanafunzi ili kuimarisha uhusiano wa kielimu
kati ya nchi hizo mbili.
“Tunaamini kuwa kwa kushirikiana,
tutaweza kuinua viwango vya elimu ya amali barani Afrika na kusaidia
vijana kupata ujuzi unaohitajika katika soko la ajira,” alisema Prof.
Mkenda.
Ziara hii ni ushahidi wa namna mageuzi ya elimu nchini
yanavyotambuliwa kimataifa, na jinsi ambavyo nchi inavyojenga nafasi
yake kama kitovu cha ubunifu na ubora katika elimu ya amali Afrika.
𝗠𝗔𝗚𝗘𝗨𝗭𝗜 𝗬𝗔 𝗘𝗟𝗜𝗠𝗨 𝗧𝗔𝗡𝗭𝗔𝗡𝗜𝗔 𝗬𝗔𝗩𝗨𝗧𝗜𝗔 𝗡𝗖𝗛𝗜 𝗡𝗬𝗜𝗡𝗚𝗜𝗡𝗘 𝗞𝗨𝗝𝗜𝗙𝗨𝗡𝗭𝗔
0 Comments