CAF WAPANDISHA PESA ZA MAANDALIZI KWA VILABU SHIRIKI

Shirikisho la mpira wa miguu Afrika (CAF) limepandisha kiwango cha hela za maandalizi kwa vilabu vitakavyoshiriki mashindano ya CAF kuanzia msimu ujao wa 2025/26.

CAF wamepandisha kutoka dola 50,000 ambazo ni zaidi ya milioni 100 kwa fedha za Tanzania hadi dola 100,000 ambazo ni zaidi ya milioni 200 za Tanzania.

Mabadiliko hayo yamekuja baada ya mkutano wa kamati ya utendaji ya CAF (EXCO) baada ya majadiliano ya kujenga kati ya chama cha vilabu vya Afrika (ACA) na rais wa CAF Dkt Patrice Motsepe .


 

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form