WAZIRI wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb)amesema safari ya mabadiliko katika Sekta ya Kilimo siyo ya kubahatisha ‘betting’ bali ni sayansi na uchumi. Ameeleza zaidi kuwa hakuna njia za mkato kwenye shughuli za kilimo, kwa kuwa bei ya zao inaamuriwa kwa sayansi na hesabu siyo kukaa mezani kucheza kamari ‘bet’.
Waziri Bashe amesema hayo wakati wa Mkutano wa hadhara wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika viwanja vya stendi ya zamani, wilaya ya Bariadi, Mkoani Simiyu tarehe 18 Juni 2025.
“Mhe.
Rais, tunaenda kujenga kongani ya viwanda (industrial park) ndani ya
Mkoa wa Simiyu ambayo litakuwa na Viwanda vidogo vya uchakataji wa
marobota na Serikali imetoa Shiling Bilioni 10 kwa ajili ya kuanza
ujenzi wa kongania hiyo ambapo Serikali ita gharama umeme, maji na
maghala. Hivyo, wawekezaji watafunga mashine tu za uchakataji,” amesema
Waziri Bashe.
Aidha, Waziri Bashe amesema kuwa zao la Korosho
limenufaisha wakulima kutokana na ruzuku hivyo ili kuongeza tija ya
uzalishaji wa Pamba, Serikali imetoa ruzuku ya mbegu na viuatilifu bure
kwa wakulima.
Pia Serikali imechukua hatua ya kusambaza
Vinyunyizi vyenye thamani ya Shilingi Bilioni 3, matrekta 205 ambapo
wakulima watachangia Shilingi 35,000 kama tozo ya kulimiwa kwa ekari.
“Msiende
kuangusha bei kwa wakulima wa Pamba kwa kuwatishia bei kama miaka ya
huko nyuma iliyoshusha bei ya zao hilo hadi shilingi 500. Kumbukeni bei
ya Pamba haiamuriwi katika mikutano ya hadhara bali ni sayansi ya
hesabu hutumika kulingana na soko la Dunia, Niwahakikishie Serikali
itawalinda wakulima,” amesema Waziri Bashe.
Hatua hiyo ni
dhamira ya Serikali kuinua zao la Pamba ili kilo 1000 iweze kupatikana
katika ekari moja; ikiwa ni pamoja na kujenga pia maghala yapatao 300 ya
kuhifadhia Pamba na mazao ya kilimo kwa ujumla.
Katika hatua
nyingine, Waziri Bashe pia amewatoa hofu wakulima wa Mbaazi kuwa mnada
wa kwanza utafanyika tarehe 20 Juni 2025 siku ya ijumaa katika wilaya ya
Bariadi na kuwataka magagaranja wafuate utararibu; kwa kuwa bei
itajulikana siku hiyo
Tags
Habari