Rais Dkt. Samia amekuwa katika ziara Mkoani Simiyu ambapo amezindua miradi mbalimbali ya maendeleo vikiwemo viwanda vya kuchakata Pamba vya Moli Oil Mills Ltd. katika wilaya ya Bariadi; BioSustain Tanzania Limited katika Wilaya ya Meatu; na Shree Rajendra Agro Industry Limited kilichopo Wilaya ya Maswa.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Kenani Kihongosi naye amepongeza hatua ya Wizara ya Kilimo kuweka Maafisa Ugani wa BBT ambao wamekuwa mkombozi kwa wakulima kwa kutoa elimu ya kilimo bora, matumizi sahihi ya mbegu na mbolea na kusimamia zoezi la upandaji kwa wakulima ambapo mavuno yameongezeka.

0 Comments