KUANZISHWA
Mineral
Access Systems Tanzania Ltd (MAST) ni Kampuni ya Kitanzania,
iliyoanzishwa mwaka 2011, ikiwa na dhamira ya kuendeleza biashara ya
madini kwa njia shirikishi na endelevu. Imekuwa ikifanya biashara ya
madini ya kimkakati (strategic minerals) ndani na nje ya nchi mfano
Zambia, Congo, Zimbabwe na South Africa, hususan shaba, nikeli na
manganese, kwa kushirikiana na wachimbaji wadogo katika mikoa mbalimbali
nchini.
UWEKEZAJI
Kiwanda cha MAST - Chunya ni matokeo ya
uwekezaji wa zaidi ya dola milioni 10 za Kimarekani (USD) ikiwa ni
uwekezaji wa ubia kati ya Kampuni ya MAST na MCC kutoka New York,
Marekani.
LENGO LA KUANZISHWA
Kuchenjua madini ya shaba yenye
kiwango cha chini 0.5 hadi asilimia 2 yanayopatikana katika eneo hilo la
Mbugani Chunya na kuyapandisha thamani kufikia hadi asilimia 75 (copper
cement) kwa kutumia teknolojia ya leaching na cementation.
UWEZO WA SASA WA UZALISHAJI
Kwasasa
kiwanda kina uwezo wa kuchakata takriban tani 31,200 za mashapo ya
shaba kwa mwezi, ambapo tani 27,200 zitatoka katika mgodi wa kampuni
hiyo ya MAST, na tani 4,000 zitanunuliwa kutoka kwa wachimbaji wadogo
nchini.
MPANGO WA UJENZI WA VIWANDA VINGINE NCHINI
MAST ina
mpango wa kujenga viwanda vingine vitatu vya uchenjuaji katika mikoa ya
Manyara-Simanjiro, Ruvuma-Mbesa (Tunduru), na Dodoma, kila kimoja
kikitarajiwa kutoa ajira zaidi ya 500 na kuchochea athari za kiuchumi
zenye thamani ya USD milioni 40 kwa mwaka.
MPANGO WA UANZISHAJI MITAMBO MINGINE
Kiwanda
kimejipanga kuanzisha mitambo maalum ya usindikaji wa nikeli kwa ajili
ya kushughulikia aina zote mbili mbale za madini ya Nikeli ambazo ni
laterite na sulfide. Hatua hii inalenga kutekeleza kwa vitendo dhamira
ya kitaifa ya kuongeza thamani ya madini yote yanayochimbwa ndani ya
mipaka ya nchi.
AJIRA ZILIZOZALISHWA HIVI SASA
Tayari kiwanda
kimetoa ajira kwa wafanyakazi 254, wakiwemo 209 waajiriwa moja kwa moja
wa MAST na 45 kupitia wakandarasi. Kati ya hao, watanzania 205
wamenufaika moja kwa moja ambao takriban ya asilimia 60 ya hao wakitoka
Mkoa wa Mbeya, Wilaya ya Chunya.
Tags
Makala