Takwimu za kidunia zinaonesha kuwa idadi ya Wajane ni takriban millioni 258 kati ya hao, Wajane 115 millioni wanadhulumiwa, wanafanyiwa ukatili, wanakabiliwa na umaskini na kutengwa na jamii.
Tanzania ina idadi ya Wajane 1,396,262 sawa na 4.4% ya Wanawake wote nchini (Sensa ya Watu na makazi mwaka 2022).
Tanzania inaungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha Siku ya Kimataifaya Wajane ambayo huadhimishwa tarehe 23 Juni kila mwaka yenye lengo la kuikumbusha jamii kudai haki za Wajane.
Maadhimisho
ya Wajane hulenga kutafakari hali zao baada ya kufiwa na wenza wao,
kuwaunganisha katika mitandao ya kupata taarifa za fursa za kiuchumi,
kijamii na uongozi.
Aidha siku hii hutumika kuelimisha kuhusu
haki zao, kupinga ukiukwaji wa haki za binadamu, kama vile kunyimwa
urithi, kufukuzwa nyumbani, kulazimishwa kuolewa, kutengwa na kukosa
msaada wa kisheria.
Tags
Habari