Timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars, imeandika historia kwa kutwaa ubingwa wa CECAFA Women's Championship 2025 baada ya kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Kenya kwenye fainali iliyopigwa kwenye dimba la Azam Complex Chamazi.
Bao la kujifunga kwa beki wa Kenya Enez Mango dakika ya 49 baada ya kushindwa kuzuia mashambulizi yaliyofanywa na Mshambuliaji wa Twiga Stars anaekipiga klabu ya Al Nassr ya kule falme za Kiarabu Clara Luvanga na kupelekea ushindi huo kwa Tanzania.Twiga Stars wamefuzu rasmi kwa AFCON ya wanawake (WAFCON), wakionyesha dhamira ya kupambana kwenye jukwaa la bara.
Rekodi ya CECAFA Women's Championship kwa Tanzania:
2016-Mabingwa
2018-Mabingwa
2025-Mabingwa (rekodi ya mataji 3)
Tags
Michezo