Mkuu wa Wilaya ya Lindi- Bi Victoria Mwanziva amekabidhi magurudumu (Matairi) kwa ajili ya gari ya Chama - CCM Wilaya ya Lindi Vijijini- katika kuunga mkono jitihada na kazi nzuri inayoendelea kufanywa na Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Lindi Vijijini inayohudumia Jimbo la Mtama-Halmashauri ya Mtama alipohudhuria kikao cha kikanuni cha Kamati ya Siasa.
Kamati ya Siasa iliyoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Lindi Vijijini Ndg. Hongonyoko kwa kauli moja imemshukuru DC Mwanziva kwa mchango wake na kumpongeza kwa namna anavyoiongoza vyema Wilaya ya Lindi na kudumisha mashirikiano kati ya chama na Serikali.
Aidha kikao hicho kimetanguliwa na utambulisho wa Katibu Mpya wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Lindi Vijijini Ndugu. Feisal Hamadi ambaye amehamia CCM Wilaya ya Lindi Vijijini.
Kamati ya Siasa ya Lindi Vijijini kwa ujumla wake imepongeza mafanikio yanayozidi kupatikana na miradi mingi ya maendeleo iliotekelezwa na Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mwisho kamati ya Siasa imeweka azimio la kuhamasisha wananchi kujitokeza katika uchaguzi mkuu ujao na kusisitiza umoja na mshikamano, uadilifu, utulivu, maadili, nidhamu na haki katika uchaguzi wa ndani ya chama.