RAIS WA YANGA ACHUKUA FOMU YA UBUNGE KIGAMBONI

 RAIS wa klabu ya Yanga, Mhandisi Hersi Said leo Jumamosi, Juni 28, 2025 amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Kigamboni kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Hersi amechukua fomu hiyo katika Ofisi ya CCM Kigamboni na amekabidhiwa na Katibu wa CCM wa Kigamboni, Stanley Mkandawire huku akitarajiwa kuchukua nafasi ya aliyekuwa Mbunge Jimbo hilo, Faustine Ndugulile aliyefariki dunia mwanzoni mwa mwaka huu alipokuwa nchini India kwa ajili ya matibabu

“Nikiwa kama mwanachama wa CCM nimekuja kutekeleza haki yangu ya kikatiba ya kupata nafasi ya kuchaguliwa na nimekuja kuchukua fomu ya kuomba ridhaa kwa kugombea nafasi ya Ubunge kuwakilisha Jimbo la Kigamboni”—amesema Injinia Hersi.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form