Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema
miongoni mwa sababu za kuongezeka kwa deni la taifa ni kutokana na fedha
ambazo zilikopwa na awamu zilizopita kupokelewa na awamu hii ya sita.
Akilihutubia
Bunge jana juni 27 Rais Samia amesema “Ni vyema tukafahamu kuwa mkopo
unaweza kusainiwa leo lakini fedha husika zikaanza kupokelewa baada ya
maandalizi ya mradi kukamilika na mradi kuanza ili lile deni au mkopo
huo uingie kwenye deni la serikali lazima serikali iwe imepokea fedha
hizo huduma au vifaa tulivyokubaliana”
“Katika awamu ya sita
pamoja na kusaini mikopo mipya lakini pia tumeendelea kupokea fedha za
mikopo ambayo ilisainiwa katika vipindi tofauti na kuongeza kiwango cha
deni la serikali”
Rais Samia amesema serikali imepokea kiasi cha shiilingi Trilioni 11.3 ikiwa ni mikopo iliyosainiwa na awamu zilizopita.
Pamoja na hayo ameeleza pia sababu zingine ni kuimaria kwa dola ya marekani jambo linalochangia kukua kwa deni la nje.
“mfano
mwezi machi 2021 kiwango cha kubadilisha shilingi ya kitanzania dhidi
ya dola za marekani ilikuwa shilingi 2298.5 wakati mwezi Machi mwaka huu
kiwango hicho kulikuwa 2650 hivyo endapo deni la serikali litatajwa kwa
shilingi za kitanzania lazima lionekane limeongezeka”
Rais Samia ameeleza kwa mwaka huu deni limeongezeka kwa zaidi shilingi trilioni 3.9 kutokana na ‘exchange rate’.
Hadi
kufikia mei 2025 deni la serikali limefikia trilioni 107.7 ambapo deni
la nje ni shilingi trilioni 72.94 na deni la ndani ni 34.76.