RAIS SAMIA AFUNGUA DARAJA LA MAGUFULI,KIGONGO-BUSISI

 Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi Daraja la J.P Magufuli kati ya Kigongo - Busisi lenye urefu wa Kilomita 3 lililopo kati ya Misungwi na Sengerema mkoani Mwanza.

 Kufunguliwa kwa Daraja la Magufuli kunakwenda kuondoa adha kwa wananchi waliokuwa wanaipata kwa miaka mingi kutokana na Vivuko kuzidiwa na idadi kubwa ya magari na abiria wanaoelekea Mikoa ya Geita, Kagera, Kigoma pamoja na nchi jirani Uganda, Burundi na Rwanda.

Ujenzi wa daraja hilo uliasisiwa na Hayati. John Magufuli, ambae alifariki Machi 17, 2021, ambapo daraja hilo likiwa limefikia 25% za utekelezwaji wake na mrithi wake, Rais Samia Suluhu Hassan amendeleza na hatimaye leo kukamilisha kwa asilimia 100.



Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form