MBIO za ufungaji bora, kiungo wa Simba, Jean Charles Ahoua ameendelea kuwakimbia washambuliaji wa Yanga, Clement Mzize na Prince Dube.
Ahoua
amefikisha mabao 16 baada ya kufunga moja dhidi ya KenGold, akiwaacha
matatu Mzize na Dube wenye 13 huku wachezaji wote hao wakibakiwa na
michezo miwili kuhitimisha msimu huu ambapo Juni 25 timu zao zitakutana
zenyewe.
Kina Mzize wanahitaji kufunga mabao matatu kila mmoja
ili kumng’oa Ahoua kileleni ikiwa hatafunga katika mechi mbili zijazo
kwani staa huyo wa Simba ana penalti nyingi ukilinganisha na nyota hao
wawili wa Yanga.
Tags
Michezo