Chama cha
Mapinduzi (CCM) wilaya ya Iringa Vijijini kimeendesha mafunzo maalum kwa
makatibu wa siasa na uenezi kutoka kata zote 28 za wilaya hiyo
yakilenga kuwaandaa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kupitia uelewa
wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025-2030.
Akizungumza
katika mafunzo hayo Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM wilaya hiyo Anold
Hezron Mvamba amewataka wenezi hao kusoma na kuielewa kwa kina Ilani ya
Uchaguzi ya chama hicho akisisitiza kuwa imegusa maeneo muhimu kama
kilimo, afya, elimu na nishati. “Ilani hii lazima iwafikie
wananchi kwa usahihi ili kufanikisha ushindi wa kishindo kwa CCM katika
uchaguzi mkuu ujao,” amesema Mvamba.
Mvamba ameongeza kuwa
mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa CCM Taifa
Rais Samia Suluhu Hassan ni ushahidi tosha wa utekelezaji mzuri wa Ilani
hivyo ni wajibu wa makatibu hao kuwa mabalozi wa kueleza maendeleo
hayo.
Kwa upande wake Katibu wa CCM wilaya ya Iringa Vijijini
Bi. Sure Mwasanguti aliwataka wenezi hao kuielewa vyema Katiba ya chama
pamoja na maelekezo mbalimbali ya chama hasa kuelekea uchaguzi Mkuu.
Mgeni
rasmi katika mafunzo hayo, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa Vijijini,
Ndugu Constantino Kihwele aliwahimiza makatibu wenezi kutambua wajibu
wao kwa chama na kuepuka kubeba wagombea kabla ya mchakato rasmi wa
uteuzi.
“Chama chetu kitapata wagombea bora watakaoiwakilisha
CCM kwa ufanisi katika nafasi zote,” alisema huku akiwahimiza makatibu
hao kuendelea kuwaeleza wananchi mafanikio ya serikali ya awamu ya sita
na kusisitiza kuwa kazi kubwa iliyofanywa na Rais Samia ni msingi wa
ushindi mkubwa wa chama katika uchaguzi ujao.
“Chini ya uongozi wa Rais Samia, bendera ya CCM itapepea kwa kura za kishindo


