CAMARA UHAKIKA KIPA BORA LIGI KUU

KITENDO cha Simba kushinda 5-0, kimemfanya kipa namba moja wa kikosi hicho, Moussa Camara kujihakikishia tuzo ya Kipa Bora wa Msimu kwa kufikisha clean sheet 18, ambazo zinaweza kufikiwa na Djugui Diarra pekee, ambaye anaweza kufanya washindi wa tuzo hiyo kuwa wawili msimu huu.

Hata hivyo, hiyo ni kama tu Diarra ambaye ana clean sheet 16, hataruhusu bao katika mechi mbili zilizobaki na Camara akashindwa kutoruhusu bao katika mechi mbili zijazo.

Hii inamaanisha Camara ameshajihakiishia kumaliza kinara, na endapo Diarra akimfikia, Tanzania itakuwa na makipa bora wawili kama England msimu huu.

Pia golikipa huyu wa klabu ya Simba anawania tuzo ya Golikipa Bora wa mwaka wa Guinea katika tuzo za CIS Media Moussa Camara anawania tuzo hiyo na Mory Keita (Hafia Fc), Mohamed Camara (Asante Kotoko), Sekou Sylla (Horoya), na Yero Diallo (Renaissance). 

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form