Na Ally Mandai.
Siku ya tarehe 30
Agosti 2025, wakati wa kampeni za mgombea wa CCM, Ndugu Dkt. Samia
Suluhu Hassan, katika eneo la Mtumbatu, Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa
Morogoro, wananchi waliomba maji safi na salama.Mgombea Dkt. Samia
aliwaahidi kuwachimbia kisima cha maji ndani ya siku mbili.
Leo,
31 Agosti 2025, utekelezaji wa ahadi hiyo umeanza rasmi. Wataalamu wa
Wizara ya Maji wamefika eneo la Mtumbatu asubuhi na wameanza kupima
miamba. Mashine ya uchimbaji itafika saa nane mchana ili kuanza kazi ya
kuchimba kisima kirefu kwa ajili ya kuhudumia wananchi wa eneo hilo.
Pichani: Wataalamu wa Mkoa na Wizara ya Maji wakitekeleza agizo la mgombea wa CCM Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan.