Wakati kampeni
za Uchaguzi Mkuu zikiendelea kupamba moto katika maeneo mbalimbali ya
nchi, CEO wa Manara TV na Mgombea Udiwani wa Kata ya Kariakoo, Haji Manara jana alipata nafasi ya kumtembelea Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania,
Sheikh Dkt. Abubakar Zuber Bin Ally, nyumbani kwake Magomeni jijini Dar
es Salaam.
Katika ziara hiyo, Manara alimuomba Mufti dua na baraka ili safari yake ya kisiasa iwe ya amani na yenye mafanikio.
Mazungumzo yao pia yaligusia umuhimu wa mshikamano wa kitaifa na kudumisha maadili ya kidini wakati wa mchakato wa uchaguzi.
Haji
Manara alisisitiza kuwa viongozi wa dini wana nafasi kubwa katika
kuhakikisha siasa zinabaki kuwa chombo cha mshikamano badala ya
mgawanyiko.
Ziara hiyo imeonekana kama hatua ya kuimarisha
heshima kwa viongozi wa dini na kuonyesha mshikamo wa kijamii katika
kipindi hiki cha kampeni.