Mariam Nassoro Kisangi amechukua rasmi fomu ya kugombea ubunge wa Jimbo la Temeke kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Hafla hiyo imefanyika katika ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, ambapo fomu hizo alikabidhiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).
Katibu wa CCM Wilaya ya Temeke, Daniel George Sai, amethibitisha kukamilika kwa zoezi la uchukuaji wa fomu kwa wagombea wote watatu wanaowakilisha majimbo ya Temeke. Wagombea hao ni Mariam Nassoro Kisangi (Jimbo la Temeke), Abdallah Chaurembo (Jimbo la Chamazi), na Kakulu (Jimbo la Mbagala). Katibu huyo alieleza kuwa chama kimejipanga kikamilifu kwa ajili ya kampeni, ambazo zinatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 28 Agosti 2025.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Manispaa ya Temeke ametoa wito kwa wagombea wote wa majimbo husika kuhakikisha wanajaza fomu za uchaguzi kwa umakini mkubwa. Aidha, aliwakumbusha kuzingatia masharti na sheria zote zinazohusu mchakato wa uchaguzi ili kuhakikisha uchaguzi huru, wa haki na wa amani.

.jpeg)
.jpeg)
