WAFUGAJI KUPATA SOKO LA UHAKIKA LA NGOZI

 Wafugaji wa Tanzania wanatarajia kunufaika na soko la uhakika la ngozi kufuatia kukamilika kwa ujenzi wa kiwanda cha kuchakata ngozi kilichopo chini ya ubia kati ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Jeshi la Magereza.


Kiwanda hicho ni sehemu ya mradi mkubwa w (KLIC) na kimekamilika kwa asilimia 100, kikisubiri kuanza rasmi uzalishaji baada ya kukamilika kwa hatua ya majaribio ya mitambo ifikapo Septemba 2025.

Katika ziara ya Bodi ya Wadhamini ya PSSSF kutembelea miradi ya Mfuko katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Bi. Joyce Mapunjo, alisema kuwa kukamilika kwa kiwanda hicho ni habari njema kwa wafugaji waliokuwa wakikabiliwa na changamoto ya soko la ngozi.

"Kiwanda hiki cha ngozi ni jibu kwa wafugaji wetu kwani tuna ngozi nyingi sana. Juhudi zifanyike ili kiwanda kiweze kufanya kazi vyema na hatimaye wafugaji wanufaike na mradi huu," alisema Bi. Mapunjo.

Kwa mujibu wa taarifa, kiwanda hicho kina uwezo wa kuchakata futi za mraba milioni 13 za ngozi kwa mwaka. Kati ya hizo, asilimia 60 ya ngozi zitachakatwa kwa ajili ya bidhaa za ngozi ndani ya kiwanda, huku asilimia 40 zikiuzwa kwenye masoko ya ndani na ya kimataifa.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Dkt. Rhimo Nyasanho, alisema uwepo wa kiwanda hicho utasaidia kuongeza thamani ya ngozi nchini na kuwapatia wafugaji soko la moja kwa moja.

“Tuweke nguvu kwenye kiwanda cha kuchakata ngozi, kwani hapa nchini tuna ngozi nyingi. Kwa uwepo wa kiwanda hiki, wafugaji wetu watakuwa na soko la uhakika,” alisema Dkt. Nyasanho.

Katika kuhakikisha ufanisi wa mradi huo, Mwenyekiti wa Bodi alishauri wabia wote wa kiwanda kukutana na kujadili changamoto zozote zinazoweza kuzuia utekelezaji wa malengo ya mradi huo. Alisisitiza kuwa kiwanda hicho kina uwezo wa kuwa mfano wa mafanikio katika Afrika Mashariki iwapo kitasimamiwa ipasavyo.

Mbali na kiwanda hicho, wajumbe wa bodi pia walitembelea miradi mingine inayotekelezwa na PSSSF jijini Arusha ikiwemo Mradi wa nyumba za makazi Oloirieni, ambao tangu mwaka 2012 umeweza kurejesha gharama za uwekezaji na kuendelea kuwa chanzo kikuu cha mapato ya Mfuko.Jengo la kitegauchumi la PSSSF Arusha House



Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form